USIKU WA SAUTI KUFANYIKA MWEZI UJAO
Onesho ka usiku wa sauti na marafiki wa kweli litakalo wakutanisha wanamuziki mbalimbali waliowahi kupiga bendi ya Diamond Sound 'Dar es Salaam Kibinda Nkoi' pamoja na wanamuziki wengine nyota nchini litafanyika mwezi ujao
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Endless Fame inayoandaa onesho hilo, Zulfa Msuya alisema Dar es Salaam kuwa, kusogeza mbele kwa onesho hilo kumetokana na baadhi ya wanamuziki kuwa safarini huku wengine wakiwa katika kazi za kurekodi na bendi zao
"Tumelazima kusogeza mbele onesho hili kwa sababu walengwa wakuu walikuwa safarini wangine walikuwa wanakazi ya kurekodi, kwa hiyo hawakuweza kuanza mazoezi kwa muda uliotakiwa,lakini sasa wamesharejea wote na wako teyari kuanza kambi kwa ajili ya siku hiyo " alisema