UPELELEZI HAUJAKAMILIKA KESI YA LULU
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imeambiwa na upande wa Jamhuri kuwa upelelezi wa kesi dhidi ya msanii wa filamu Elizabeth Michael (18) maarufu ‘Lulu’anayekabiliwa na mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba (28) bado haujakamilika
Kesi hiyo ilitajwa jana mbele ya Hakimu Augustina Mmbando ambapo upande wa Jamhuri unaendelea kuieleza mahakama hatu za upelelezi wa kesi hiyo, kwamba bado unaendelea
Hakimu Mmbando alisema kesi hiyo itatajwa Oktoba 8 mwaka huu na mshtakiwa ataendelea kukaa mahabusu
Aidha kwa mujibu wa Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA), Lulu hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji lakini mara upelelezi wake utakapokamilika itahamishiwa Mahakama Kuu Tanzania , Kanda ya Dar es Salaam