Baada ya kitendo cha wasanii wawili wanaotamba kwenye tasnia ya filamu nchini Wema Sepetu na Aunt Ezekiel kupanda jukwaani huku wakionyesha sehemu kubwa ya maungo yao mapya yazidi kuibuka kwenye sakata hilo huku baaadhi ya wasanii wa tasnia hiyo kuonyesha kukelwa na kitendo hiko
Kwa upande wake msanii anayefanya vizuri katika soko la filamu nchini Jacque Pentzel alisema kuwa alishangazwa na kitendo hiko cha wasanii hao kupanda jukwaani na kuonyesha maungo yao wazi wazi bila ya aibu . Alisema kuwa wakati unafanya kitu lazima uangalie unachokifanya kina matokeo gani kwenye jamii yako
"Kwa upande wangu mimi siwezi kufanya hivyo na kama nasema siwezi kufanya hivyo basi hilo jambo kwangu si zuri ,na naamini hata hao walifikilia kabla ya kufanya kitendo hiko na waliamini ni kizuri ndio maana wakafanya" alisema
Aliongezea kuwa hana shida na soko la filamu kutokana na kitendo hiko kwani anaamini kuwa kila msanii anawashabiki wake,
Kwa upande wake msanii anayefanya vizuri katika tasnia hiyo pia ya filamu nchini Rose Ndauka anasema kuwa kama msanii ni kioo cha jamii hivyo lazima kila unachokifanya uifikilie jamii yako wataipokeaje tukio lolote kabla haujafanya
Anasema kuwa wasanii wanatakiwa kusimama kwenye misingi na maadili ya nchi yetu pamoja na maadili ya kazi za sanaa ili kukuza tasnia ya sanaa isipoteze muelekeo
"Kitendo kilichotokea sijakielewa kabisa sijui hata kwa nini waliamua kufanya hayo ambayo wamefanya bila ya kufikilia utu wao na heshima kwa jamii yao ni kitendo cha aibu kiukweli" alisema Rose