Google PlusRSS FeedEmail

PINGAMIZI ZA LULU KUSIKILIZWA LEO




Mahakama ya rufaa leo inatarajia kuanza kusikiliza pingamizi za kuchunguza umri wa msanii maarufu wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu’

Maombi hayo yatasikilizwa mbele ya jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo ambao ni Jaji Benard Luanda, Jaji January Msoffe na Jaji Katherine Oriyo

Lulu anakabiliwa na kesi ya mauaji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo anadaiwa kumuua msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili 7 mwaka huu Sinza Vatican Dar es Salaam

Umri wa msanii huyo umezua utata baada ya mawakili wanaomtetea kudai kuwa ana miaka 17 na si 18 kama hati ya mshtaka inavyoonyesha , na kuomba kesi yake isikilizwe katika Mahakama ya Watoto

Mahakama Kuu ilikubali kuchunguza umri wa mshitakiwa huyo lakini siku iliyotajwa kuanza kufanyiwa uchunguzi wa umri halali wa mshatakiwa huyo upande wa mashtaka uliitrifu mahakama hiyo kuwa umewasilisha Mahakama ya Rufaa maombi ya marejeo ya uamuzi huo

Jaji Fauz Twaib ndiye aliyotoa uamuzi wa kukubali kuchunguza umri huo lakini kutokana na upande wa mashtaka kuwasilisha maombi yao mahakama ya rufaa aliahirisha kuendelea na uchunguzi wa umri wa msanii huyo hadi Mahakama ya Rufaa itakapotoa uamuzi wake

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging