Google PlusRSS FeedEmail

ASIA IDARIOUS KUSHIRIKI ABAYA FASHION SHOW




MBUNIFU  mkongwe nchini, Asia Idarious atashiriki katika onyesho la kipekee lililobatizwa jina la Abaya Fashion Show and Luncheon litakalofanyika Oktoba 12 ambalo litakuwa maalumu kwa wanawake tu.

Idarious anasema baada ya kufanya maonyesho ya mengi huko Marekani safari hii atashiriki katika onyesho hilo la kipekee kuonyesha ukongwe wake katika fani hii.

"Kwa miongo mitatu niliyokuwemo ndani ya fani hii naweza kusema nimejifunza mambo mengi nilipokuwa Marekani, nilifanya 'fashion show' katika miji mbalimbali ambayo kwa kweli imenijenga na ujuzi wake sasa nitauonyesha siku hiyo," anasema Asia.

Asia anasema kuwa hii itakuwa mara ya kwanza kwake kufanya onyesho la aina hii, lakini kutokana na uzoefu alionao anasema anaamini litakuwa bora.

"Mimi ni mbunifu mkongwe kuliko wote, nimeshafanya shoo ambazo huwezi kuzihesabu, Abaya itakuwa ya aina yake kwani kutokana na mpangilio mzima wa tukio lenyewe," anasema Asia.

Mwenyewe anasema anajivunia kwa kuweza kufanya maonyesho makubwa nchini ikiwemo Lady in Red na Khanga ya Kale.

Onyesho hilo linalodhaminiwa na Red Onion, An Nisa na Valley Spring litafanyika katika mgahawa wa Red Onion uliopo katika jengo la Haidery Plazer jijini Dar.

Tukio hilo la aina yake lililopewa jina la Abaya Fashion Show Luncheon litafanyika kwa muda wa saa tatu tu, kuanzia saa tisa na nusu mchana mpaka saa kumi na mbili.

Mbali na Asia mbunifu mwingine nguli, Mustafa Hassanali naye ataonyesha Abaya zake ambazo mapema mwaka huu alizionyesha huko Dakar, Senegal.

Kwa kuwa sherehe hii ni maalum kwa wanawake tu, Mustafa atawakilishwa na mwanamke katika onyesho hilo.

Aidha mmiliki wa lebo ya Kidoti, Jokate Mwegelo atakuwa mshereheshaji huku wanamitindo mahiri kama Fiderine Iranga na Warda Walid wakiwa miongoni mwa watakaaonyesha mavazi hayo siku hiyo.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging