Wasanii wa filamu za Tanzania Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wametakiwa kufika katika ofisi za Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),kujieleza kuhusiana na kudaiwa kuonesha picha za utupu kwenye mitandao
Inadaiwa wasanii hao ambao ndio kioo cha jamii walianika picha zinazoonesha maumbile yao huku zingine zikionesha sehemu ya makalio kwenye mitandao ya kijamii
Akizungumza Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Taff, Wilson Makubi alisema wasanii hao wamepelekewa barua ya kikao hicho na kuwataka wafike katika ofisi za shirikisho hilo leo saa 7 mchana ili kujieleza walichokifanya
Alisema shirikisho pamoja na wasanii wengine katika tasnia hiyo wamehuzunika na tabia hiyo iliyofanywa na wasanii hao hivyo leo watajieleza na litatolewa tamko dhidi yao
Alisema wamekaa na Baraza la Sanaa la Tanzania (BASATA) ambalo wamepewa maagizo ya kuwashughurikia wasanii watakayoishushia thamani tasnia hiyo ya filamu