Google PlusRSS FeedEmail

NDAUKA ANAKUJA NA 'SPECIAL COVER'



Msanii wa filamu mwenye mvuto wa aina yake nchini Rose Ndauka yuko jikoni kuipika filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la 'Special Cover' ambayo amecheza kwa umahiri mkubwa akiwa amevaa uhusika wa watu wawili tofauti

Msanii huyo ambaye yupo makini na kazi zake alizungumza hivi karibuni alieleza kuwa special cover ni filamu itakayokuja kubadilisha soko la filamu nchini kutokana na ubora wa kazi hiyo

Alisema kuwa kwa sasa yuko chimboni akiitengeneza filamu hiyo ambayo itatoka hivi karibuni na kuwasisistiza wadau wa filamu wakae mkao wa kuipokea kazi yake

Ndauka alisema kuwa filamu hiyo yenye uwalisia na mazingira ya tanzania na imebeba maudhui yanayoendana na jamii yetu hivyo anaamini kuwa itatikisa soko la filamu nchini Tanzania na kuleta mabadiliko makubwa kwa wadau wa filamu



Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging