CHRIS BROWN : SIJARUDIANA NA RIHANNA
Mwimbaji wa pop na R&B Chris Brown amesema hajarudiana na mpenzi wake wa zamani kama ilivyoripotiwa katika vyombo vya habari
Hivi karibuni Brown alitangaza kuachana na mpenzi wake Karrueche jambo lililotafsiriwa kuwa anataka kuwa karibu na Rihanna
Karrueche Tran na Chris Brown wameonekana tena wakiwa pamoja huko Kaskazini mwa Hollwood, pia wiki iliyopita Chris na Rihanna walionekana kaskazini mwa West Hollywood katika klabu moja ya usiku, lakini wakati wa kutoka kila mmoja alitoka kivyake
Lakini katika tukio kama hilo Brown ameonekana akienda katika klabu hiyo akiwa na Karrueche








