Google PlusRSS FeedEmail

NISHA KUIGIZA NA BONGO DAR ES SALAAM



Msanii nyota kwenye tasnia ya filamu nchini Salma Jabu 'Nisha' mbali na kuonekana kutoka katika anga za filamu ataanza kuigiza katika tamthilia ya kupitia kundi maarufu la Bongo Dar es Salaam

Wakizungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam wadauwa wa tasnia hiyo mara baada ya kumuona Salma katika hali ya kurekodiwa katika sehemu ya tasnia hiyo wiki iliyopita wamesema wamempongeza kwa maamuzi aliyoyafanya kwa kuanza kushiriki maigizo

"Kwa kujiigiza katika anga za uigizaji msanii huyo mara tamthilia hiyo itakapoanza kuonekana moja kwa moja atakuwa amejiongezea umaarufu mwingine kwani kila wiki atakuwa anaonekana luningani " alisema Rashid Nassor ama Chid Mzee wa Mbele

Alisema kundi hilo mara baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu kwa sasa lipo katika hatua ya uandaaji na uchukuaji wa picha za tamthilia ya kundi na muda tu litaanza kuonekana katika anga za luningani na kuanza kuonyesha mvuto kama ilivyokuwa awali


This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging