HUSSEIN MACHOZI : BAADHI YA WASANII WANAOENDA KUFANYA SHOO NJE YA NCHI WANAFANYA SEBULENI
Nyota anayetisha katika anga za muziki wa Bongofleva nchini Hussein Rashid, maarufu kwa jina la Hussein Machozi amesema hayuko teyari kupelekwa nchi za nje kwa ajili ya kufanya shoo za sebuleni
Machozi alisema shoo za aina hiyo hazina maana yoyote kwa msanii kwa vile hapati nafasi za kuonyesha uwezo wake na kutimiza malengo yake ya kimuziki
Kwa mujibu wa Machozi wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya nchini wanaoalikwa kwenda kufanya maonyesho nje ya nchi hawapati nafasi ya kuutangaza muziki wao kimataifa kwa vile maonyesho hayo huwa ni ya watu wachache
Machozi alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha Star Tv kuhusu maendeleo na Mustakabali wake kimuziki








