Google PlusRSS FeedEmail

DJ DEA WA PRO 24 ANAJIVUNIA KUTUMIA TURNTABLE SYSTEM&SERATO


Fani ya muziki inazidi kukua siku hadi siku kwa kuongezeka kwa idadi kubwa ya watu kujua muziki pamoja na kuufanya muziki kuwa sehemu yao ya maisha

Ukizungumzia tasnia ya muziki bila shaka utamzungumzia dj ambae kazi yao kubwa ni kuutambulisha muziki kwa jamii nzima inayotuzunguka, pamoja na kumtambulisha msanii wa muziki huo

Unapowataja ma Dj wa Pro 24,hauwezi kuliacha jina la 'Dj Dea' ambaye ni moja kati ya ma dj wanaokuja kwa kasi katika tasnia hiyo huku akiwa na mchango mkubwa katika kulinga'risha jina la Pro 24

Alex Ashery ndiyo jina alilopewa na wazazi wake, ila kutokana na msukumo mkubwa wa kazi na kuwa na kitambulisho kitakachomtambulisha yeye pamoja na kazi yake akajikuta anapewa jina la 'dJ-DEA'

DJ-Dea alianza kazi ya kuwa dj mnamo mwaka 2008 akiwa anapiga muziki katika kumbi mbalimbali ikiwemo Emma Entartainment

Dea alifanya kazi hiyo sehemu tofauti tofauti kwa takribani miaka 4 ndipo alipojiunga na kundi zima la Pro 24 dj's Anasema kuwa alivutiwa na kundi hilo la Pro 24 kwa kile kitendo cha wao kama kundi kufanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu huku wakiwa na nia moja ya kufika katika ngazi ya kimataifa tofauti na makundi mengine

Dea anasema kuwa mbali na ufanisi wa kazi pia  kikubwa kilichomfanya ajikute akisukumwa kujiunga na kundi hilo ni hile hali ya kutaka kupata nafasi ya kufanya kazi hiyo ya muziki katika hali iliyo kuwa  na mafanikio kwa kupata muongozo

Anasema kuwa mengi amejikuta akizidi kuyafahamu baada ya kuingia katika kundi hilo kwani hapo mwanzo alizoea kutumia mbinu za zamani ambazo sasa hazina nafasi katika soko la burudani

Anafunguka kwa kusema kuwa matarajio yake ni kuwa dj wa kimataifa, kwa kupitia kundi hilo atatimiza ndoto zake alizotarajia kwani ndani ya pro 24 ni chuo cha muziki kwake

Anaendelea kuelezea kuwa hauwezi kutarajia makubwa kisha ukabweteka, hivyo juhudi na kuongeza maarifa ndio kitu cha msingi ili uweze kufanikisha malengo yako

Dea anasema kuwa kikubwa wanachokifanya wao ni kufanya mazoezi ya kutosha kabla hawajafanya shoo hali hiyo inawajenga na kuwaongezea uwezo wa kujiamini na ujuzi wa kile wanachokifanya

Mbali na hilo mazoezi ni kitu ambacho kinawafanya kila siku kufahamu ni nyimbo gani mpya imetoka na ipi inafaa kupigwa katika kumbi za starehe 'Club' na zile zisizofaa kupigwa maeneo hayo,Anasema kuwa kwa kazi yao anakutana na changamoto kubwa, hususani kwao kwani sasa wanapiga nyimbo ambazo ziko kwenye mtindo wa video hivyo kila siku ni lazima waangalie ni video gani mpya iliyoingia katika fani hiyo

Dea ambaye amekili kuwa na mafanikio makubwa baada ya kuingia katika kundi hilo, akusita kutaja baadhi ya mafanikio yake yaliyotokana na pro 24 kwa kipindi kifupi tangu ajiunge hapo

Anasema sasa ameweza kuwa na uwezo wa kumiliki mashina yake ambayo inampa uhuru katika kuendeleza shughuri zake za muziki huku akiwa na uwezo wa kufanya mazoezi mahali popote

Mbali na hilo pia anasema kuwa kundi la Pro 24 Djs wanatumia vifaa vya kisasa ambavyo vinaendeshwa na komputa tofauti na makundi mengine ya ma dj, Anaeleza kuwa amekuwa na uwezo wa kutumia Techics Turntable System na Serato hivyo ni vifaa vya kisasa kabisa ambavyo vimemfanya kuwa na uwezo mkubwa na kukuza kipaji chake cha muziki na kufikia lengo la kuwa wa kimataifa

"Nimeachana na kutumia Cd kupiga muziki, dj wa ukweli unatumia Technics Turntable System na Serato hii inaonyesha ni jinsi gani ulivyokuwa na uwezo wa kucheza na mashine zenye hadhi ya kimataifa" alijinadi

Dea ambaye pia anapiga muziki sehemu mbalimbali za Club nchini Tanzania ingawa kwa sasa anapiga muziki katika kituo cha Terevisheni cha Taifa (TBC 1) kinachorushwa kila siku ya Alhamisi kuanzia saa 5 usiku huku akionekana kuwa mahiri katika ufunguzi wa shoo hiyo

Anaelezea kuwa yeye hupangwa katika ufunguzi wa shoo hiyo kwa kile kinachodaiwa uwezo wake na ubunifu wake kwa kuweza kuisoma hadhira yake

Anasema kuwa uwezo huo ameupata katika kundi hilo la pro 24 kwa kufanya mazoezi kwa bidi huku kila siku akifikilia kuongeza ubunifu ili awe na mvuto mkubwa katika kazi zake, Anaelezea kuwa anauwezo wa kufanya shoo kubwa za wasanii wanaokuja nchini kwa ajili ya kufanya shoo na wasanii wa hapa nyumbani

Dea ambaye ambaye mbali na kuwa dj yeye pia ni mcheza mpira ambaye anamudu kucheza namba 7 kama winga, Anasema kuwa mbali na kuwa dj pia yeye ni mcheza mpira mzuri ambapo anatumia muda wake wa mapumziko kwa kucheza mpira hali hiyo inamsababisha kujikinga na vishawishi ambavyo wanakutana navyo

Anasema kuwa anaheshimu kazi yake kwani inampatia kipato ambacho ndicho kinachomsaidia kuendesha maisha yake ya kila siku hivyo dj kwake ni kazi ambayo yeye anaheshimu

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging