DNA AWAPAGAWISHA MADEMU WA BONGO
Msanii kutoka nchini kenya anayetamba na kibao cha 'Unamaswali ya Polisi' amewapagawisha mashabiki ndani ya ukumbi wa Club Bilicans katika uzinduzi wa usiku wa Club ulioandaliwa na Pro 24 Djs pamoja na Televisheni ya Taifa (TBC ONE )
Msanii huyo ambaye pia alionekana kuwa kivutio kikubwa kwa mabinti hali iliyomsababisha kupanda mzuka kwa kuingia katika stage ya mashabiki na kuanza kucheza nao
Akizungumza baada ya shoo hiyo msanii huyo alisema kuwa hakutegemea kama mashabiki wa bongo wangempokea kwa hali nzuri na kuweza kuziimba nyimbo zake
Alisema kuwa hali hiyo imempa faraja kubwa na kugundua kuwa anawashabiki pande zote na ambao wanafwatiria kwa umakini kazi zake