DOGO JANJA AMZIMIA DNA
Dogo Janja msanii anayekuwa kwa kasi kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya amekiri 'kumzimikia' msanii wa kutoka nchini Kenya DNA kwa kile kinachodaiwa anapenda kazi zake zilizoambatana na ubunifu wa hali ya juu
Dogo Janja aliyasema hayo baada ya kumaliza kupiga shoo ya 'ukweli ndani ya ukumbi wa Club Bilicans katika uzinduzi wa Usiku wa Club ulioandaliwa na TBC I pamoja na Pro 24 Dj's
Alisema kuwa anajikuta anamzimia msanii huyo na kwake imekuwa ni faraja kubwa kufanya shoo pamoja katika stage moja huku wakiwa wamepata nafasi ya kuzungumza
Dogo Janja alisema kuwa alikuwa na ndoto za kukutana na msanii huyo, hivyo kwake imekuwa ni njia ya kukamilisha ndoto yake
Dongo Janja ambaye kwa sasa yupo katika kundi la watanashati baada ya kutoka Tip Top Connectio