ISHA MASHAUZI AMZIMIKIA ROMA MKATOLIKI
Umahiri ulionyeshwa na msanii bora wa Hip Pop nchini Tanzania Ebrahim Mussa 'Roma Mkatoliki' kwa kuweza kuimiliki 'stage' ya Dar Live jijini Dar es Salaam katika tamasha la East Africa Pamoja Concert lililoandaliwa na Pro 24 Dj's uliwavutia mashabiki akiwemo Isha Mashauzi na kusababisha kupanda jukwaani na kupiga naye picha
Isha ambaye ni msanii wa taarabu alivutiwa na msanii huyo wa Hip Pop, Roma kwa kile kinachodaiwa kuwa kazi yake ni nzuri ikiongozwa na mashahiri yaliyojaa ubunifu wa hali ya juu
Akizungumza na Maisha baada ya shoo Roma alisema kuwa si kitu kigeni msanii wa taarabu kuipenda kazi yake kwani ukifanya kitu kizuri kila mtu atakipenda kwa nafasi yake
"Ingawa Isha alikuwa amemaliza kufanya shoo lakini aliniambia anaisubili shoo yangu ndio aondoke, mimi nachukulia ni matokeo ya kazi yangu kuwa na mashabiki wa aina mbalimbali" alisema Roma
Akizungumzia kwa upande wa uandaaji wa tamasha alisema kuwa kazi nzuri inafanyika kwa kuleta idadi kubwa ya wasanii wengi kutoka nje, huku idadi ikiwa ndogo ya wasanii wa nyumbani kupata mialiko ya shoo nje
Alisema kuwa hiyo ni changamoto kwa waandaaji kwa kuangalia ni jinsi gani ya kuboresha uandaaji wa matamasha kama hayo na wasanii wa hapa wapate nafasi kubwa ya kufanya shoo nchi za jirani
Aliongezea kuwa ingawa hawapati nafasi hiyo lakini wanawashangaza wasanii wa nje kwa ujuzi walionao kwa kuweza kumiliki stage kwa umahiri wa hali ya juu