Werasson aliondoka Wenge BCBG baada ya mzozo wa pesa na uongozi baina yake na JB Mpiana, alipoondoka alikwenda kuanzisha WMMM na vijana wake akatafuta vijana akawatengeneza wakaiva hatimaye WMMM ikatisha balaa.
SG Eliot Mandobe ambaye alijulikana kama Secretary General, au Le Secrétaire Général de l’orchestre alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na kukubalika ndani ya kundi la WMMM. Lakini kizuri hakidumu jamaa alikimbia bendi kwa kashfa ya Human Trafficking na kukimbilia Canada hasa baada ya Show ya Zamba Playa ambapo alisemwa kuwa alikimbia akiwa na maelfu ya dola ambazo alikusanya toka kwa watu ambao aliwaahidi kuwatafutia VISA ya kwenda Ulaya, Canada na Marekani kupitia mgongo wa bendi.
Suala la Human Trafficking liliwahi kumgarimu Shumbu Wemba Dio Papaa Wemba Miezi kadhaa jela huko Ufaransa na Fellix Wazekwa aliwahi kutandikwa miezi kumi gerezani huko Braxelles kwa kosa kama hilo ambapo kuna wakati VISA za wanamuziki wa Congo zilisumbua kwani Tshengeni iliamua kupitia upya maombi yoote ya VISA toka kwa wanamuziki wa CONGO. Mandobe baadaye alijiunga na familia yake ikiwa ni mke na watoto ambao walitangulia kuishi huko, Nakuacha na kibao hiki ambacho utamuona vizuri Mandobe akikamua akiwa na Tata Mukulu Werrason Ngiama Makanda ndani ya Wenge Musica Maison Merre.








