Google PlusRSS FeedEmail

SISTER MWASU AIIBUKA KIDEDEA TUZO ZA MAMA SHUJAA WA CHAKULA



TUZO za Mama Shujaa wa Chakula 2021-2013, zimekamilika juzi usiku baada ya Sister Martha Mwasu kutoka Kondoa kuibuka mshindi wa kwanza na kujinyakulia zawadi ya vifaa vya kilimo vyenye thamani ya shilingi milioni 10

Sister Mwasu aliibuka kidedea kwa kuwaangusha washiriki wenzie 13 walioingia katika kinyanganyiro hicho kutokana na kuwa na juhudi na ubunifu mkubwa aliouonyesha kwa kipindi cha wiki mbili alizokuwa akiishi katika kijiji cha Maisha Plus zilizomsababisha kupata kura nyingi kutoka kwa wananchi

Nafasi ya pili ilishikiliwa na Bi.Emilian Eligaisha kutoka Karagwe na kupewa zawadi ya vifaa vya ujenzi vya milioni 3, nafasi ya tatu ikichukuliwa na Bi. Tatu Abdi Kutoka Lushoto ambapo alipewa shilingi 700000

Akizungumza wakati akikabidhi zawadi kwa mshindi wa tuzo ya hiyo Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bw. January Makamba alisema kuwa kuna kila sababu ya kuboresha mazingira rafiki kwa wakulima hususani kwa akina mama kwani shunguli zote za kilimo zinafanywa na wanawake

Alisema kuwa Fikra dume, sera dume, pamoja na mipango dume huzaa matokeo dume hii inasababishwa na kuleta utofauti wa jinsia katika utekelezaji na uwajibikaji wa maendeleo

Makamba alisema kuwa asilimia 95 ya chakula tunachokula kinazalishwa na akina mama, cha kushangaza asilimia 99 ya wasiyozalisha chakula ndio wanaomiliki ardhi, na kusababisha kuwa na unyanyasaji wa kijinsi unaomgusa moja kwa moja mwanamke

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging