Google PlusRSS FeedEmail

LINAH AKANUSHA KUJIENGUA THT



Msanii kutoka Nyumba ya Vipaji (THT) Lina Sanga, 'Linah' aka Ndege Mnana amekanusha uvumi uliokuwa ukivumishwa kuwa amejitoa THT kwa madai kuwa anawapisha chipukizi ili wapate nafasi ya kutengeneza majina na kukuza vipaji vyao

Msanii huyo amekanusha uvumi huo na kudai kuwa hawezi kutoka THT kwa madai kuwa wamemtoa mbali na wamefanya jitihada kubwa za kumfikisha hapo alipo sasa

Akizungumza na jalida la Maisha Linah alisema kuwa ameshangazwa na uvumi huo kwani hajawahi kufikilia kutoka THT , zaidi atajiimarisha katika nyumba hiyo ya kukuza vipaji ili aweze kufikia malengo yake ya kimuziki

"Nimeshangazwa na uvumi huo na sijui kwa nini walinivumishia habari hiyo, mimi siwezi kutoka THT  nitabaki hapa mpaka malengo yangu yatimie, wamenitoa mbali kimuziki hivyo siwezi kwenda kokote na hakuna sehemu nyingine itakayonifaa zaidi ya hapa nilipo" alisema Rinah

Akizungumzia upande wa maisha yake kiujumla, Linah alisema kuwa yupo katika mahusiano ambayo anatarajia siku moja hivi karibuni kufunga ndoa na kujenga familia bora

Alisema kuwa anamshukuru mungu amepata mwanaume anayemjali na kuijali kazi yake ya muziki, hivyo yupo naye bega kwa bega kwa kila hatua yake ya muziki ili kuhakikisha anafanikiwa

"Mwanaume ambaye niko naye ananipenda na anaipenda kazi yangu hivyo anaijali na kushirikiana na mimi kwenye kila tukio la muziki ili kuifanya kazi yangu iwe bora zaidi" alisema Linah

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging