WEMA NA AUNT, WAIOMBA MSAMAHA JAMII
Hatimaye ma diva wa filamu nchini Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wameomba msamaha kwa jamii kwa kile kitendo kilichotokea kwa kupanda jukwaani huku wakionyesha sehemu kubwa ya maungo yao
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Wema Sepetu alisema kuwa wanaomba msamaha kwa jamii nzima kwa kitendo kilichotokea kwani anaamini kuwa wameikosea jamii kwa ujumla ikiwa wao ni kioo cha jamii
Msamahaa huo umekuja baada ya Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF) kushinikiza na kukipigia kelele tabia hiyo kwa madai kuwa wanaishushia hadhi tasnia ya filamu nchini
Pamoja na hayo uongozi wa TAFF liliwaandikia barua za onyo wasanii hao kwa kitendo hicho walichokifanya huku Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lililaani tabia hiyo ya kudharilisha sanaa kwa ujumla







