NEY WA MITEGO: HUWEZI KUZUNGUMZIA BURUDANI YA MUZIKI BILA YA KUWATAJA PRO 24 DJ'S
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ney wa Mitego alionekana kuwa kivutio kwa mashabiki waliohudhuria tamasha la 'East Africa pamoja Concert' lililoandaliwa na Pro 24 Dj's Katika ukumbi wa Dar Live jijini Dar es Salaam
Alionekana kuwa kivutio kikubwa na kuibua hisia tofauti za mashabiki baada ya kupanda jukwaani kwa kuwashutikiza kwani hakuwa kwenye ratiba ya usiku huo
Akizungumza baada ya kushuka jukwaani Ney alisema kuwa alivutiwa kuja kwenye shoo hiyo kwani Roma ambaye ndiye alikuwa yuko kwenye jukwaa ni mtu ambaye avutiwa na kazi yake
Alisema kuwa amepata faraja baada ya kuona mashabiki wamelipuka kwa furaha kubwa hali hiyo inamsababisha kuona kuwa kazi yake ina kubalika katika jamii
Akizungumzia juu ya tamasha hilo alisema kuwa huwezi kuzungumzia burudani bila ya kuwataja Pro 24 Djs ambao sasa wako kwa ajili ya kuifanya sanaa ya muziki kuwa ya kimataifa
Alisema kuwa hapo mwanzo walishazoea ni kundi la watu fulani kuandaa matamasha, na wengine wapo kibiashara hivyo kusababisha kupoteza dira ya muziki nchini
Ney anasema kuwa pro 24 wapo kwa ajili ya kutoa burudani na anaamini kuwa watafanya makubwa zaidi katika upande wa kukuza muziki na kiwango cha burudani nchini
Ney akizungumzia kuhusiana na nyimbo zake kujaa mafumbo, anasema kuwa yeye anaimba ukweli na daima atasimama kwenye ukweli ili jamii ibadilike "Mimi naimba ukweli hivyo nitasema ukweli kama umefanya kitu nitakisema kwenye nyimbo, na atakayeguswa atabadilisha tabi yake " alisema Ney
Ney alipanda jukwaani kwa kushtukiza wakati msanii Roma Mkatoliki akifanya shoo