NICKI MINAJ, MARIAH CAREY WAINGIA KWENYE BIFU LA MAISHA
Mambo yamezidi kuwa mabaya baina ya majaji wapya wa shindalo la kusaka vipaji vya kuimba la 'American Idol' Mariah Carey na Nicki Minaj, huku uvumi ukidai kwamba Mariah ameongeza ulinzi kwa sababu amehofia usalama wake dhidi ya Nicki Minaj kufuatia kubwatukiana wakati wa mchujo wa shindano hilo
Katika kipindi cha televisheni cha "The View" mtangazaji Barbara Walters alibainisha kuwa alizungumza na Mariah ambaye alimueleza kwamba ameongoza walinzi zaidi baada ya Nicki kudaiwa kusema, "kama ningekuwa na bastola ningemshuti yule mala****"
Mariah amesema ameguswa na swala hilo , alisema Walters hafikirii kwamba kuna jambo lolote litakalotokea, lakini Nicki hatabiriki na Mariah hayuko teyari kutoa upenyo hivyo amekodi ulinzi
Nicki hajaomba radhi lakini tangu wakati huo wawili hao wamekutana na waandaaji wa shindalo hilo la kuimba na majaji wenzao
Kulikuwa na mkutano Jumatano asubuhi baada ya mkutano huo Nicki alimwambia Mariah "nakupenda lakini twaweza kugombana tena " Mariah alijibu "hapana hatuwezi"
Mtangazaji Walters aliendelea kusema kutokana na kauli hiyo Nicki, Mariah alisema hajisikii amani tena lakini ataendelea kufanya kazi zake kama jaji wa mashindano