Google PlusRSS FeedEmail

OMOTOLA JALADE ANAYETINGISHA TASNIA YA FILAMU NIGERIA







Kama utataja majina kumi ya wasanii wa kike katika tasnia ya filamu nchini Nigeria, hutakosa kuligusa jina la mwanadada Omotola Jalade

Hii ni kutokana na uwezo mkubwa alionao katika tasnia hiyo na kuwa miongoni mwa waigizaji wa kike waliogiza filamu nyingi na kupata mafanikio makubwa

Mbali na tasnia ya filamu mwanadada huyo utamtaja pia katika fani ya muziki kutokana na umahiri wake katika sekta hiyo

Historia inatuonyesha kuwa Omotola Ekeinde Jalade ni mtoto wa familia ya watoto watano ya Bwana na Bibi Shola Jalade, ambao kwa sasa wote ni marehemu na ana kaka wawili Tayo na Bolaji Jalade

Omotola ambaye kwa sasa anasoma ya Utawala katika chuo cha Teknolojia cha Yaba, kilichopo mjini Lagos alifunga ndoa na Kapteni Matthew Ekeinde katika ofisi za msajili wa ndoa yao ndani ya ndege kutoka mjini Lagosi hadi nchini Benini April 19, 2001 ambapo hadi sasa wanandoa hao wana watoto wanne

Inaelezwa kuwa Omotola alianza kung'ara katika kijiji cha Nollywood baada ya kufyatua filamu aliyoipa jina la 'Mortal Inheritance' aliyoicheza mwaka 1995 ambako aliigiza kama mgonjwa mwenye matatizo ya ugonjwa wa Sickle-Cell ambaye anapigania uhai wake licha kuwa anafahamu hatapona ,ingwa siku alipona na kupata mtoto na hatimaye aliendelea kuishi

Filamu hiyo amabyo ilikubalika iliweza kupata tuzo na tunaelezwa kuwa hadi sasa bado inafahamika kuwa ni miongoni mwa filamu bora nchini Nigeria

Tunaelezwa kuwa tangu kipindi hicho mwanadada huyo hakuweza kugeuka nyuma ambapo aliendelea kufyatua filamu kali kali kama vile 'Games Women Play' 'Blood Sisters', 'All my life' na nyinginezo kabala ya mwaka 2005 kujitumbukiza kwenye kazi ya muziki

Katika fani ya muziki mwaka 2006 alifyatua albamu yake aliyoipa jina la 'Gba'

Zifuatazo ni filamu ambazo msanii huyo ameweza kuzifyatua

Ties That Bind (2011)
A private Stom
Ije: The Journey (2010)
My Last Ambition(2009)
Beyonce&Rihanna(2008)
Temple of Justice(2008)
Tomorrow Must Wait(208)
Yankee Girls(2008)
Careless Soul(2007)
Desperate Sister(2007)
Final War(2007)
Sand in My Shoes(2007)
Sister's Heart(2007)
The Prince of My Heart(2007)
The Revelatio(2007)
Titanic Battle(2007)
Tota War(2007)
Brave Heart(2005) hizo ni baadhi ya filamu alizocheza msanii huyo

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging