EXTRA BONGO YAONGEZA NGUVU YA WANENGUAJI
Bendi ya muziki wa dansi ya Extra Bongo imewatambulisha rasmi wanenguaji watatu kutoka bendi ya African Star 'Twanga Pepeta na FM Academia 'wazee wa ngwasuma' ambao wamejiunga na bendi hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja
Wanenguaji hao ni Maria Salome,Sabrina Mathias kutoka twanga pepete na Titi Mwinyi wa FM Academia
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa utambulisho huo Mkurugenzi wa bendi hiyo alisema kuwa wamefikia maamuzi hayo baada ya kupokea maombi kutoka kwa mashabiki wao ambao wanahitaji wanenguaji wapya wa kike ili kunogesha safu hiyo
Aliongezea kuwa baada ya kuwatambulisha wanenguaji hao bendi hiyo pia itawatambulisha rasmi kwa mashabiki wake katika ukumbi wa New White House baada ya hapo watawapeleka mkoani Mwanza








