Jennifer Lopez alionyesha umbo lake wakati alipohudhuria
hafla ya hisani ya timu ya mchezo ‘American Football’ huko Puerto Rico
Akiwa amevalia kaptula fupi nyeusi na jezi nyekundu ya
mchezo wa ‘American Football’ nyota huyo aliacha wazi miguu yake mirefu wakati
akicheza na bintiye Emme Anthony na
boifrendi wake kijana mwenye umri wa miaka 25, Gasper Smart
J-Lo (43) na boifrendi wake huyo ‘dogodogo’ ambaye ni dansa
wake walisherehekea mwaka mmoja wa mahusiano yao mwezi Oktoba mwaka huu
Walionekana pamoja katika duka la vito la Tiffany&Co,
nchni Australia mapema mwezi huu na kuzua uvumi kwamba huenda muimbaji huyo
akaolewa kwa mara ya nne. Ndoa zake tatu zilivunjika