MUUMIN ADHAMIRIA MAKUBWA VICTORIA SOUND
Mwanamuziki Mwinyuma Muumini amejaribu tena kulinda kipaji chake cha uimbaji kwa kujiunga na bendi ndogo ya Victoria Sound ambayo sasa iko kambini mjini Mtwara ikiandaa nyimbo mpya
Muumini amejiunga bendi hiyo akitokea African Stars 'Twanga Pepeta' aliyodumu nayo kwa zaidi ya mwaka mmoja huku akisema kuwa hatua yake hiyo ni kama kuhama timu kubwa ya soka na kwenda mchangani
Kauli hiyo ya muuimbaji huyo imetokana na ukweli kwamba bendi ya Victory Sound haina jina kwenye fani ya muziki wa dansi kama ilivyo twanga pepeta iliyojizolea sifa tangu mwisho mwa miaka ya 90
Anaamini kwamba uwezo wake aliyokuwa nao kwenye muziki wa dansi utaifanya bendi hiyo kuwa miongoni mwa bendi kubwa zinazotamba na hivyo kuifanya kujizolea sifa na mashabiki wengi