Google PlusRSS FeedEmail

KINONDONI WAIBUKA WASHINDI MIONDOKO YA 'KWAITO'


Vijana wa kinondoni waibuka kidedea katika mashindano ya kucheza miondoko yenye asili ya Afrika ya Kusini inayojulikana kwa jina la 'Kwaito' baada ya kuwashinda vijana wa Ukonga Gongolamboto

Mashindano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam 'Club Shemshi' Gongolamboto yaliyoandaliwa na Pro 24 Djs huku vijana wa Kinondoni kuibuka vinala wa miondoko hiyo

Vijana wa Gongolamboto walionekana kuwaogopa vijana wa Kinondoni kwa kutokana na aina ya uchezaji wao ambao ulionyesha vijana hao wanauzoefu wa miondoko hiyo

"Watoto wa Gongo la Mboto wanaogopa kucheza kwa sababu hawajui wameshazoea miondoko ya kizamani sisi ndiyo kila kitu" alisikika mshabiki wa Kinondoni akisema

Mashinado hayo yaliandaliwa na Pro 24 djs ikiwa ni sehemu ya kutimiza neno lao la Utamu Night ambapo wanapiga muziki kila siku ya Ijumaa mahali hapo

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging