KUTOKANA na kuwa na wimbi la waimbaji wengi wa Kikongo katika bendi za Tanzania muimbaji mkongwe ambaye pia ni mkurugenzi wa bedi ya Extra Bongo 'wazee wa kizigo' Ally Choki amefichua siri ya wakongo
Moja ya siri hiyo ni uwezo na umakini wa kazi unaonyeshwa na waimbaji hao dhidi ya waimbaji wa hapa nyumbani ndiyo sababu kubwa inayochangia baadhi ya bendi nyingi kufanya kazi na waimbaji hao
Alizungumza hayo na safu hii jijini Dar es Salaam Choki aliweka wazi kuwa waimbaji wa hapa nyumbani wanalewa sifa wanazosifiwa na mashabiki na matokeo yake wanaharibu kazi hivyo wanaona ili waendelee kuwa na mashabiki wengi ni lazima wachanganye radha tofauti
Choki aliongezea sababu nyingi inayosababisha hali hiyo ni maswala ya kibiashara kwani kazi ya muziki na sawa na kazi nyingine hivyo wanaajili kulingana na kipaji na uwezo wa mtu na jinsi gani muimbaji huyo anaheshima na kazi yake pamoja na kuithamini
"Unajua muziki ni biashara kama ilivyo biashara nyingine hivyo lazima uwe na mtu mwenye maslahi na kazi anayoifanya ili kuiboresha kazi yako" alisema Choki
Aliongezea kuwa kwa upande wa Kongo wanamuziki hao wanashindwa kupata bendi nyumbani kwao kutokana na kuwa waimbaji wengi kuliko bendi zilizopo hivyo nayo ni sababu moja wapo inayosababisha waimbaji hao kuhamia bendi za Tanzania
Kwa upande wake rapa wa bendi ya Twanga pepeta Mirinda Nyeusi alielezea sababu zinazowafanya kuhamia bendi za hapa nyumba ni kupewa nafasi ya kufanya kazi tofauti na bendi za kwao
Alisema kuwa bendi za kongo zipo nyingi ila kupata nafasi ya kufanya kazi kwenye bendi hizo ni tatizo hivyo wanalazimika kutafuta bendi sehemu nyingine ili waweze kuingiza kipato








.jpg)