HATIMAYE msanii wa bongofleva Ney wa Mitego ageukia upande wa pili na kuamua kuimba nyimbo za mapenzi huku akijinadi kuwa yeye ni mzee wa mabinti
Msanii huyo ambaye amezoeleka kusikika akiimba nyimbo za 'kuwaponda'baadhi ya wasanii wa bongo movi huku akionyesha kukereka na baadhi ya vitendo wanavyovifanya ikiwemo na mavazi ya nusu uchi pamoja na kujihusisha kwenye mapenzi zaidi ya mwanaume mmoja
Akizungumza na Safu hii Ney wa Mitego alisema ameamua kuanza kuimba kwani ni msanii wa pekee mwenye uwezo wa kuimba pamoja na kufanya Hip Hop na vyote akavimudi
Alisema mbali na hilo kumudu kufanya vizuri pande zote mbili pia kwa sababu anawajali mabinti hivyo ameamua kuanza kuimba ili mabinti kupanda radha ile anayohisi kuwa wameikosa kwa kipindi chote ambacho alisimama kuimba
"Mimi ni msanii wa pekee niliyekuwa na uwezo wa kuimba na Hip Hop kwa pamoja hivyo kwa sasa nimeamua kuachana na maswala ya kuzungumzia ukweli wa maisha ya watu hususani wasanii wa bongo movi sasa niko kwenye mapenzi zaidi" alisema Ney wa Mitego
Aliongezea kuwa pia anaangalia upande wa biashara muziki unalipa wapi zaidi hivyo inamlazimu abadilike kulingana na hali ya kibiashara
Ney wa Mitego ameachia nyimbo mbili mpya zinazozungumzia maswala ya mapenzi nyimbo hizo zinajulikana kwa jina la Ndolena na Utavuna ulichokipanda








