Lady Gaga amebainisha kuwa hataendelea na matamasha kwa kuwa hawezi hata kusimamam kutokana na maumivu makali anayoyapata katika mguu
Staa huyo mwenye umri wa miaka 26 amesema kwamba maumivu hayo yamempa ugonjwa mwingine wa moyo kwa kuwa amelazimika kuwaangusha mashabiki wake
Mwanamuziki huyo alisema kuwa amevumilia maumivu katika mguu huu kwa muda mrefu na kuupuuzia huku akiendeelea na matamasha, lakini sasa hali yake imekuwa mbaya
"Moyo unaniuma sana kwa kuwa nimewaangusha mashabiki wangu,ninawaahidi kuwa nitarudi jukwaani mara baada ya kupona" anasema Gaga