CIARA: MIMI SITAKI BIFU
Ciara hana mpango wa kuingia katika 'bifu' la kwenye mtandao wa kijamii ambalo Rihanna na wapambe wake wameliibua hivi karibuni
Wakati wakifanya mahojiano ya kupromoti albamu yake ijayo ya 'One Woman Army' Ciara alisema , "Nadhani ni masihala na inachekesha mimi sijali nimetulia wanaweza kufanya wanachotaka, mimi akili yangu iko kwingine kabisa " alisema Ciara huku akiongezea kumtakia mafanikio Rihanna katika kazi yake "Rihanna anamambo mengi mno ya kufanya tena yenye maana kuliko haya"








