MOJI OLAIYA ATAKA KUACHANA NA MUMEWE
Muigizaji wa Nollywood, Moji Olaiya ambaye pia ni binti wa mwanamuziki maarufu wa Nigeria, Victor Olaiya amesema kuwa hali ni mbaya sana katika ndoa yake hivyo hana budi kutengana na mume wake
Olaiya alisema kuwa aliona kuwa kuolewa ni kitu rahisi sana, lakini ukweli ni kwamba kukaa katika ndoa ni suala gumu na linalohitaji umakini hasa linapokuja suala la kula na kuvaa
Katika mahojiano yake na mtandao wa Nollywood, olaiya aliweka wazi kuwa maumivu ya siri yaliyopo katika ndoa yake huku akieleza kuwa maisha ndiyo yanayomfanya atengane na mume wake na kamwe hawezi kubadili msimamo








