KIM KARDASHIAN ABADILI MUONEKANO WA MAVAZI
Kila wakati mama mtarajiwa Kim Kardashian hujitokeza kwa umma huku akiwa katika muonekano wa tofauti wa kimavazi, kinapowashangaza watu ni pale mama mtarajiwa huoyo alipoacha kuvaa nguo zake za kubana pamoja na suruali na kuanza kuvaa pamba mpya maalumu kwa ajili ya wajawazito jambo ambalo wengi limewafurahisha na kumsifia kuwa sasa ameanza kuelewa nini maana ya ujauzito
Taarifa zilizofika Hollywood zilieleza kuwa mwanamitindo huyo ambaye kwa sasa ni mke wa mwanamuziki Kanye West mwishoni mwa wiki iliyopita alihudhuria misa akiongozana na Kris Jenner huku akiwa amevalia gauni kubwa na la heshima








