Kimberley Walsh amefuata nyayo za muimbaji mwenzake katika bendi ya zamani ya Girls Aloud ambayo imesambaratika, Cheryl Cole kwa kutoa kitabu cha wasifu wa maisha yake
Baada ya miaka 10 ya kutumbuiza pamoja mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ameahidi kuelezea jinsi kundi lao la Girls Aloud lilivyokuwa
Mwezi uliopita mwishoni mwa maadhimisho ya miaka 10 ya kundi hilo lilitangaza kuvunjika kwake "Watu wamekuwa wakinitaka nielezee historia yangu kwa mara nyingine sasa, lakini si kuhisi kama ilikuwa ni wakati muafaka kwa kipindi hicho wakati nilikuwa bado nipo ndani ya bendi hiyo pamoja na wenzangu" alisema Kimberley
Machi mwaka jana mwimbaji mwingine wa bendi hiyo alitoa kitabu alichokipa jina la 'Tell-all'ambacho ndani yake ilibainisha maelezo juu ya maisha yake ya ndoa na mwanasoka nyota wa England anayechezea Chelsea








