TOM CRUISE AVUNJA NDOA YAKE
Muigizaji na mtayarishaji mahili wa filamu nchini Marekani Tom Cruise hatimaye kwa mara ya kwanza amevunja ukimya na kueleza jinsi alivyoshtuka baada ya kufunguliwa mashitaka ya kuombwa talaka na mkewe wa zamani, Katie Holmes
Taarifa za Holmes na Cruise kutengana na mke wake baada ya kuishi pamoja kwa miaka mitano ziliibuka Juni mwaka jana na majaji wakavunja ndoa yao jijini New York Agosti mwaka jana
Kwa mujibu wa mtandao wa E.Online , Cruise alivunja ukimya huyo katika mahojiano na kituo cha televisheni nchini Ujerumani, kwa kusema kuwa hakutarajia kama angetengana na mkewe








