WESLEY AWEKWA CHINI YA ULINZI NYUMBANI KWAKE
Nyota wa filamu wa hollwood, Wesley Snipes ametolewa jela nchini Marekani baada ya kutumikia adhabu ya kifungo kutokana na kosa la kukwepa kulipa kodi
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 50 alifungwa katika gereza la Pennsylvania mwaka 2010 kutokana na kosa hilo la ukwepaji wa kulipa kodi
Hata hivyo baada ya kutoka gerezani mkali huyo wa filamu za mapigano ataendelea kuwa katika kizuizi nyumbani kwa miezi minne mingine ijayo ili akamilishe kifungo cha miaka mitatu alichopewa
Snipes aliyekuwa nyota wa filamu lukuki lakini filamu iliyomaarufu zaid ni ile ya Vampire Hunter, mwendesha mashtaka wa Marekani alisema muigizaji huyo alishindwa kufanya marejesho ya kodi kwa miaka 10 hivyo alikuwa na deni la mamilioni ya dola kwa jimbo la Texas








