MUZIKI UNAKATAZA UONGO KWA WOTE
Mwanamuziki Jay Quayson amezungumzia muziki wake mpya wa 'Game Over' kuwa ni funzo kwa watu wenye rika zote, alisema kuwa kwenye kila sekta kuna tabia ya uongo hasa mapenzi na mmoja kati yao akistuka kila kitu kinakuwa kimekwisha haribika
Msanii huyo amesema kuwa amejifunza mengi kupitia kazi ya kutunga mashairi ya nyimbo zikiwemo nyimbo za injili, wasanii wenye uzoefu wa kuona nini wanafanya na mashabiki wanataka nini na ndio maana amekuja na nyimbo yenye ujumbe kama huo