PROFILE : BI. KIDUDE
Jina Kamili : FATMA binti Baraka
Jina la kisanii : Maarufu kwa jina la Bi Kidude, ni miongoni mwa wasanii wanawake wachache ambao ni magwiji wa muziki wa taarabu nchini,
Amezaliwa : ni mzaliwa wa Zanzibar lakini asili ya kabila lake ni Mmanyema kutoka Mkoa wa Kigoma, magharibi mwa nchi.
Umri : Miaka 113
Ana watoto wangapi ? : Hajabahatika kupata mtoto ingawa aliwahi kuolewa mara mbili
Muziki alianza lini ? : Mkongwe huyo wa muziki amekuwa muimbaji tangu miaka ya 1920 akiwa ni mfuasi wa Sitti Bin Saad mmojawapo wa waimbaji wa mwanzo kabisa wa taarabu visiwani Zanzibar.
Kazi ya muziki : Bi. Kidude aliweza kuteka soko la muziki hususani wa mwambao kwa kutunga mashahiri yaliyobeba ujumbe wa mahaba pamoja na mafumbo kwa lugha ya kiswahili yenye lengo la kufikisha ujumbe wake kwa mashabiki wake
Nyimbo zilizofanya vizuri : Nyimbo zake zilizoweza kufanya vizuri ikiwemo Yalait, Muhogo wa Jang’ombe, Kijiti, Arebaba na Machozi ya huba
Asili ya jina lake : Kwa mujibu wa taarifa ya vyombo tofauti vya habari Bi. Kidude alielezea asili la jina lake kuwa alipewa na mjomba wake wakati alipozaliwa kwa sababu alikuwa na umbile dogo.
Safari yake ya muziki : Akiwa na umri wa miaka 13 hakuwa na jinsi bali kukimbilia Tanzania bara(Tanganyika enzi hizo) ili kuepuka kuozeshwa kwa nguvu. Akiwa Tanzania bara alizunguka kila kona ya nchi akiwa muimbaji katika makundi mbalimbali ya muziki wa taarabu likiwemo lile maarufu la Egyptian Musical Taarab. Baadaye alihamia nchini Misri kwa kifupi kabla hajarejea kisiwani Zanzibar mahali ambapo umauti wake ulipomkuta.
Tuzo za muziki : Amewahi kupokea tuzo mbalimbali mwaka 2005 , nchini Uingereza,ambapo alipokea tuzo yenye heshima kutoka World Music Expo (WOMEX) kwa mchango wake katika muziki na utamaduni wa Zanzibar. Katika kinyang’anyiro hicho aliwashinda wanamuziki mahiri kama Peter Gabriel, Miriam Makeba na wengineo.
Aliyeibua kipaji chake : Mtu wa kwanza kuthamini kazi za kumtafuta hadi kufika alipo alikuwa Rais mstaafu wa Tanzania wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.
Ziara ambazo amewahi kufanya : Aliwahi kufanya ziara nchini Uingereza kwa Malkia Elizabeth II , ambao alipewa zawadi ya kidani cha dhahabu ikiwa ni moja ya kuthamani kazi yake. ziara ya pili ya muimbaji huyo ilikuwa nchini Ujerumani ambapo aliweza kusimama kwenye majukwaa na kutumbuiza.
Ameishi : Kutokana na umahili wa uimbaji wake pamoja na kuwa na mashahiri yenye ubunifu huku akikitangaza kiswahili aliweza kuishi nchini Ajipshini (Egyptian) kwa miaka tisa kutokana na kazi hiyo ya muziki
Kazi nje ya muziki : Ameweza kuwa mmoja wa wasanii waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya Malaria iliyokwenda kwa jina la 'Zinduka' kwa kuhudhuria kampeni hiyo aliweza kukonga nyoyo ya Rais Kikwete
Sifa ya Bi. Kidude : Kuimba kwa kutumia kichwa na dhati ya moyo wake kwenye kuimba kwani kubana au kuibadili sauti wakati wa kuimba si sahihi, inamtoa mwimbaji kwenye uhalisia wake.
Uvutaji wa Sigara : Sifa yake nyingine kuwa alikuwa na uwezo wa kuvuta sigara ambapo kwa siku alikuwa anauwezo wa kuvuta pakiti moja kwa siku tatu huku sauti yake ikiwa bado ipo imara
Hali ya ugonjwa wake : Bi. Kidude alianza kuumwa mwishoni mwa mwaka jana akiwa akisumbuliwa na maradhi ya sukari, ambayo ni maradhi yake ya muda mrefu ila yalizidi baada ya kukiuka taratibu za vyakula








