ROBBIE AMKANA ADELE HADHARANI
Robbie Williams amekanusha taarifa kwamba ameungana na Adele kurekodi wimbo mpya, huku akisisitiza kwamba hakuna mpango wowote wa kutoa kibao na nyota huyo wa muziki wa soul
Williams amekuwa karibu na Adele baada ya mke wake Ayda Field kuanzisha urafiki na mdada huyo na mapema mwaka huu wote walijifungua watoto
Taarifa za hivi karibuni zilibainisha kwamba wawili hao wapo kwenye mikakati ya kutoa kibao cha pamoja lakini sasa Williams ameeleza wazi hana mpango wowote wa kufanya au kushirikiana kimuziki na mshindi huyo wa tuzo za Oscar








