UJAUZITO KUTOMZUIA HALLE BERRY KUONEKANA KWENYE MUVI
Star wa muvi wa kike kutoka Hollywood, Halle Berry amesema kwamba ujauzito hautomzuia kurekodi picha ya filamu yake mpya ya 'Stormin X-Men Days of Future Past'
Star huyo wa filamu (46) anatarajia kupata mtoto wake pamoja na mchumba wake raia wa Ufaransa Olivier Martinez lakini hana mpango wa kuchukua likizo ya mateniti
Berry amesisitiza kwamba atatokea kwenye filamu ijayo ya X-Men ambayo itaanza kupigwa picha zake baadaye mwaka huu, lakini amesema hatojihusisha kwenye sehemu ya mapigano








