Muigizaji Monalisa Shinda amesema kuwa hafikirii kuolewa hivi karibuni kutokana na kilichomkuta kwenye ndoa yake ya kwanza, alisema hapo kabla hakuwa makini kujua nani anafaa kuwa mume na nani rafiki kutokana na kutoka kwenye familia ya kifalme ambayo ilikuwa ni lazima aolewe bila ya kujali na mwanaume gani ilimradi aonyeshe ustarabu lakini sasa kitu hicho hakiwezi kutokea
"Niliwahi kuolewa na nikaachika sitaki kitu hicho kinirudie tena kama itatokea kuolewa basi iwe na mwanaume sahihi ambaye nitakuwa nimemchagua na kujua mazuri na mabaya yake kitu kitakachonipa unafuu wa kumuudu"








.jpg)