Google PlusRSS FeedEmail

JINA LA WOLPER LAFANYIWA UTAPELI


MSANII wa filamu nchini Tanzania Jacqueline Wolper amewajia juu baadhi ya watu wanaotumia jina lake vibaya kwa ajili ya kutapeli mashabiki wake kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook.

Msanii huyo amewajia juu baada ya kupokea taalifa kwa baadhi ya mashabiki wake wakimpa pole baada kuonekana kuhitaji atumiwe hela kwa ajili ya kutatua tatizo lake lililompata akiwa nje ya Dar es Salaam.

Taalifa hiyo ya kuomba msaada ya kutumiwa shilingi lakimoja ilitumwa kupitia mtandao ya kijamii na baadhi ya watu waliofungua ukurasa wa facebook na kujidai kuwa wao ni Wolper.

Akizungumza jijini Dar Wolper alisema anashangaa watu wanaotumia jina lake kwa ajili ya kufanya utapeli kitu ambacho kwake kinamshangaza na hajui hali hiyo imetokea kwa sababu gani

Alisema ni kitendo cha udharilishaji kinachofanywa na matapeli hao wameshazoea kutumia majina ya masupastaa kuwatapeli mashabiki wao.

"Mimi nashangaa sana kwa nini baadhi ya watu wanatumia jina langu vibaya kwa kufanya utapeli jamani na sasa yamekuwa mazoea baadhi ya wasanii wenzangu ambao pia wanamajina makubwa nao wanalalamika hivyo hivyo jambo ambalo siyo zuri kuchafuana " alisema Wolper

Wolper aliongezea kwa kuwataka mashabiki wake kuwa hatumii ukurasa wa Facebook wala Twitter hivyo mashabiki wake wanatakiwa kuwa makini na matapeli hao.

Umeibuka mtindo wa baadhi ya watu kutumia majina ya wasanii katika mitandao ya kijamii kwa nia ya kufanya utapeli .



This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging