Google PlusRSS FeedEmail

JE JAYMOE KUACHANA NA MUZIKI, KUWA MPIGA PICHA??


"PICHA ni moja ya jambo linalofikisha habari kwa jamii,picha inaweza kusimama pekee yake na ukagundua nini kinachozungumzwa" hayo ni maneno yanayosemwa na msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Jumaa Mohamedy 'Jaymoe Mchopanga' na mwandishi wa habari hii.

Jaymoe mbali ya kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya pia anajishungurisha na maswala ya upigaji picha huku akiamini kuwa siku moja kuwa mpiga picha wa kimataifa.

Jaymoe anaamini kuwa mpiga picha bora anauwezo wa kutengeneza video bora kwa upande wa muziki, hivyo kutokana na juhudi zake za kuwa mpiga  picha bora anaamini ataleta mageuzo katika upande wa utengenezaji wa video za muziki hapa nchini.

Jaymoe ambaye anahisi kukosekana kwa wapigapicha bora ndio inapelekea kukosa video zenye ubora tofauti na nchi jirani ambapo wao kwa upande wao wameweza kufanya vizuri kwa upande huo.

Anaamini kupitia kitengo cha kupiga picha atafanikiwa kuwa mtengeneza video bora za muziki ambapo hivi sasa anahisi baadhi ya video hizo hazitendewi haki kutokana na kukosa ubora.

Jaymoe ambaye ameanza safari yake ya muziki alipokuwa shule ya sekondari ingawa aliweza kujulikana kwa jamii mnamo mwaka 2001 baada ya kundi la wateule kukubalika kwa jamii.

Jaymoe ambaye ametokea katika kundi la wateule, aliweza kushirikishwa na kutokana na nyimbo inayojulikana kwa jina la 'Ulingoni' ambayo ilibeba jina la albamu ya kwanza ya msanii Solo .

Jaymoe ambaye aliweza kuikamilisha albamu yake ya kwanza akiwa chini ya studio za Bongo Records huku P- Funk akiwa ni mtayarishaji wa nyimbo zake ambapo nyimbo ambayo ilizidi kumpa umaarufu ilijulikana kwa jina la 'Mvua na Jua' .

Single ya Maisha ya Boding ni nyimbo ambayo bado inaendelea kumpa umaarufu Jaymoe ambapo kilichoimbwa katika nyimbo hiyo ni ualisia wa maisha wanayoishi wanafunzi wengi waishiyo boding.

Jaymoe ambaye mara nyingi hupenda kutumia zaidi muda wake akiwa nyumbani na siyo kutoka anaamini kuwa kusihi ndani huku akitumia computar kwa ajili ya kuongeza vitu tofauti tofauti ni njia pekee inayomuondoa na makundi mbalimbali ambayo anahisi yanaweza kuhatarisha maisha yake kwa kuiga vitu visivyofaa.

Jaymoe ambaye anamini zaidi kuvaa nguo zenye rangi ya kuvutia huku akiwa makini na fashion anaamini kuwa kupendeza ni moja ya kuongeza mvuto na muonekano sahihi., Jaymoe hajabahatika kuoa wala kupata mtoto ingawa kwa sasa anatamani kupata mtoto

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging