MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Taikuni Ally 'Mchizi Mox' baada ya kimya kirefu ameamua kurudi tena kwenye 'gemu' kwa kutoa ngoma mpya inayojulikana kwa jina la 'Piga makofi'.
Msanii huyo ambaye alitamba kwenye gemu la muziki huo kwa kipindi cha miaka ya 2000, ameamua kuingia tena studio akiwa chini ya mtayarishaji Lamar ambapo nyimbo hiyo itamrudisha tena kwenye gemu hilo wakati alikuwa ameshapotea.
Akizungumza na jarida hili Mox aliweka wazi juu ya ukimya wake kuwa umetokana na miangaiko ya maisha na kuangalia upende mwingine wa maisha unavyokwenda.
Alisema alijaribu katika masuala ya kuwa projduza lakini ilishindikana kwa kushindwa kutimiza malengo yake kutokana na changamoto alizokutana nazo kwa upande huo.
Aliweka wazi kuwa nyimbo anayoitoa ndiyo itakayomrudisha tena kwenye gemu hilo huku akiwapa burudani mashabiki wake walioikosa kwa kipindi kirefu