Google PlusRSS FeedEmail

VIFO VYA WASANII VYAHAMIA KWA WAZAZI, PROFESSA JAY AFIWA NA MAMA YAKE


Msanii nguli wa muziki wa HipHop nchini Tanzania, Pro. Jay aka Jay wa Mitulinga, amefiwa na mama yake mzazi usiku wa kuamkia leo kutokana na ajali. Mama yake msanii huyo alikuwa katika matembezi yake huko Kimara jijini Dar es Salaam, ndipo lilipotokea gari kusikojulikana na kumgonga.

Kwa mujibu wa ndugu ambaye hakutaka kutajwa jina, mama huyo alikimbizwa hospitali ya Tumbi Kibaha, na madaktari na manesi wa hospitali hiyo walipigana kuokoa maisha ya mama huyo lakini hawakufanikiwa na kisha mama huyo kupoteza maisha.

Wakati huo huo, msanii mwingine wa bongo fleva, Z Anto  naye amepoteza mama yake mzazi katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, jana.

Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging