Google PlusRSS FeedEmail

NEY WA MITEGO ATOKA NA SALAAM ZAO , AMCHANA ZITTO AKAE MBALI NA BONGO FLEVA

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ney wa Mitego amezidi kujipatia umaarufu huku akiendelea kushika chati miongoni mwa wasanii wanaongoza kuimba nyimbo zinazoibua ukweli kwa baadhi ya mambo yanayotendeka kwa jamii. Katika mashahiri yake, rapa huyo anahoji uhalali wa kazi zinazofanywa na mawaziri vizuri, pamoja na uhalali wa kuwepo wabunge wa viti maalumu bungeni. Msanii huyo ambaye leo anaachia ngoma mpya inayojulikana kwa jina la 'Salaam zao', ameandika mashahiri ya kumpa salaam Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuachana na masuala ya muziki wa bongo fleva na ajikite zaidi kwenye siasa. Mashahiri hayo yametokana na kile kinachodaiwa kuwa mbunge huyo kuanzisha kundi la Kigoma All Stars na kulitelekeza. Rapa huyo amemtumia salamu, mbunge huyo kuwa ni vyema aachane na bongo fleva na kujikita zaidi kwenye siasa, kwani huko ndiko kunakomfaa zaidi. Ney wa Mitego hakuishia hapo bali alitoa salamu kwa Rais Kikwete, kuhusu vurugu zilizoibuka hivi karibuni mkoani Mtwara zilizosababishwa na gesi. Kutokana na vurugu hizo, rapa huyo amejaribu kugusia suala hilo na kuliweka wazi kuwa "wananchi wa Mtwara hawataki tena korosho, bali wanataka gesi yao hivyo mtawaua kwa mkongo'to". Ney wa Mitego amejaribu kuwa mbunifu kwa kutumia mashahiri yake kufikisha ujumbe kwa watu anaOwakusudia kwa kuwataja jina mmoja mmoja, huku akiamini kuwa kwa kutumia njia hiyo atakuwa amesaidia jamii yake kwa kiasi kikubwa. Msanii huyo hakuishia hapo, pia alitoa salamO kwa Rita Poulsen ambaye anaendesha mashindano ya kusaka vipaji vya wasanii ya Epiq Bongo Star Seach (EBSS). Alisema hali za washindi wa mashindano hayo ni duni kulinganisha na zawadi wanazoshinda, kutokana na mashahiri hayo anaamini kila upande utaangaliwa vizuri ili kuboresha.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging