Google PlusRSS FeedEmail

MARIE STOPES YAJITOKEZA KUDHAMINI REDD'S MISS TANZANIA

SHIRIKA lisilo la kiserikali Marie Stopes (MST) yajitosa kuwa mdhamini mwenza katika kinyanganyiro cha Redd's Miss Tanzania 2013, ambapo ni moja ya tukio linalowashirikisha vijana zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na washiriki wa shindano hilo wakati wakati akisaini mkataba huo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa shirika hilo Bw. Johnbosco Baso alisema kuwa sababu ya kudhamini shindano hilo ni kupata nafasi ya kuelimisha  vijana juu ya matumizi ya njia za uzazi wa mpango.

Alisema kuwa kuwaelimisha vijana hao kuwa na matumizi sahihi ya uzazi wa mpango ili kuepuka mimba katika umri mdogo ambapo itawasaidia kutimiza malengo na ndoto zao za baadae.

Baso aliweka wazi kuwa Tanzania ina asilimia 16 ya vijana walio katika umri wa uzazi wanaotumia njia za kisasa za uzazi wa mpango, ingawa takwimu zinaonyesha vijana 8000 waliacha shule kwa sababu ya mimba za utotoni kwa mwaka 2010.

Aliweka wazi kuwa elimu hiyo pia itawasaidia vijana kuepuka utoaji wa mimba usio salamaa unaopelekea vijana wengi kupoteza maisha.

Takwimu zinaonesha kuwa Tanzania ni kati ya nchi zinazoongoza kwa idadi kubwa ya vifo vitokanavyo na uzazi ambapo kila siku wanawake 26 hupoteza maisha, huku vifo hivyo asilimia 19 vinachangiwa na utoaji wa mimba usio salama.

Alisema kuwa watatoa elimu kwa washiriki hao ambapo watamchagua mshiriki mmoja ambaye atakuwa balozi wao na kufanya naye kazi ya kuelimisha jamii juu ya matumizi sahihi ya njia za uzazi wa mpango.





This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging