Google PlusRSS FeedEmail

MCHIZI MOXIE PROFILE

Jina kamili :  Taikuni Ally

Jina la Kisanii : Mchizi Moxie  hilo ndio jina linalomtambulisha kwenye sanaa ya muziki  wa hip hop , ni miongoni mwa vijana ambaye alijiunga na fani ya muziki wa kizazi kwa ajili ya kuendeleza kipaji chake pamoja na kuinua kipaji chake.

Alianza safari yake ya muziki lini ?: Mchizi Mox alianza safari yake ya muziki akiwa masomoni kwa kujiunga na bendi ya shule, kuimba pamoja wanafunzi wenzake, huku akiwa na ndoto ya msanii mkubwa nchini.
Mchizi Mox aliamini juhudi ndizo zitakazomfanikisha mafanikio yake, kutokana na hilo aliamua zaidi kujikita katika mambo ya sanaa hata kupiga ngoma mbalimbali alipokuwa masomoni.

Ushirikiano alioupata : Akielezea historia yake kwa ufupi msanii huyo aliweka wazi kuwa, aliamua kujiunga na na mambo ya sanaa ya muziki wa kizazi kipya huku akipata ushirikiano kutoka kwa wazazi wake.

Kabla ya kundi la Wateule alitokea wapi? : Kabla ya kuunda kundi la Wateule, Moxie aliweza kufanikiwa kutoa single iliyojulikana kwa jina la 'Watoto wa mitaani' nyimbo iliyobeba ujumbe na kuelimisha jamii juu ya kudhibiti na kupunguza watoto wa mitaani. Aiweza kufanikiwa kurekodi nyimbo hiyo kwa msaada wa mama yake ambaye alimpa ushirikiano wa kwenda studio kurekodi ikiwemo kumlipia gharama zote za studio.

Safari ya muziki ilianza wapi ? : Baada ya muda Moxie aliweza kunga'ra akiwa na wenzake Jafarray pamoja na Jaymoe kwa kushinda katika mashindano ya kuibua vipaji vya muziki ambapo waliteuliwa kuwa ni kundi bora la Hip Hop.

Jina la Wateule lilianza kipindi gani ? : Hapo ndipo kundi la 'Wateule' lilipoanza katika studio ya bongo records, baada ya kufika katika studio hizo washindi hao kwa ajili ya kurekodi nyimbo ikiwa zawadi ya ushindi huo ndipo jina la wateule lilipozaliwa.

Safari ya muziki alianza lini ?: Msanii huyo alianza safari yake ya muziki mnamo 2000, pamoja na kuunda kundi hilo la wateule na kufanikiwa kutoa 'single' iliyokuwa inawatambulisha katika jamii.

Undani wa kundi la Wateule : Baada ya muda kidogo kundi hilo lilivunjika ambapo kila mmoja alianza kufanya kazi kwa mtindo wa pekee yake, hivyo Moxie alibaki kwa muda bila ya kutoa nyimbo yoyote kwenye jamii hali hiyo ilimpa changamoto kwa mashabiki wake.

Baada ya kuvunjika kwa kundi : Baada ya kimya cha muda mrefu Moxie aliendeleza kundi hilo la Wateule kwa kutoa nyimbo iliyojulikana kwa jina la 'Watu kibao' miaka 2001 ambapo nyimbo hiyo iliibua hisia kwa mashabiki walioisahau kundi la wateule.Aliweza kufanya vyema katika mambo ya muziki huku ndoto zake ni kuendelea kuwa msanii mkubwa, aliweza kufanikisha malengo yake kwa kutoa single nyingine ambayo ilimtambulisha Mox katika suala zima la muziki.

Nyimbo iliyomtambulisha kwenye gemu : Nyimbo ya 'Mambo vipi' ilikuwa ni jibu kwa Moxie ambapo aliweza kuibua na kuteka hisia za mashabiki wake huku akiendelea kuongeza mashabiki lukuki kutokana na ujumbe pamoja na aina ya uimbaji wa nyimbo hiyo huku sauti yake ikiendelea kuwa mvuto ndani ya nyimbo.

Mapokeo ya wimbo Mambo vipi : Mambo vipi, ilimuongezea mashabiki lukuki huku, pamoja na kuongeza imani kwa wasanii wenzake huku baadhi yao wakiwa na kiu ya kushirikiana nao katika kazi ya muziki.

Anachokipenda: Moxie anajivunia mvuto wa sauti yake ambayo imemfanya kumuongezea kufanya kazi na wasanii wengi huku baadhi yao wakiamini kuwa ubora wa sauti yake ndiyo inaweza kuboresha nyimbo anazoshirikishwa.

Anapenda nini kwenye kazi: Moxie  ambaye amefanya kazi za kushirikishwa na wasanii wengi hapo mwanzo, sasa ameweka bayana msimamo wake wa kutofanya kazi za kushirikishwa kwani anaona hazina faida kwake.Moxie baada ya ukimya wa muda mrefu sasa anajipanga kurudi tena kwenye gemu kwa kuachia albamu yake ya pili ambayo ataipa jina la 'Goli la pili na mwisho wa mchezo' ikiwa ndio albamu yake ya mwisho huku albamu yake ya kwanza aliipa jina la 'Goli la kwanza'

Msanii huyo aliweka wazi kuwa hana mpango wa kuendelea kutoa albamu kwani albamu hizo hazilipi ila anayoitoa ni ya mwisho na kuendelea kubaki kutoa single.Moxie ameachia nyimbo inayokwenda kwa jina la Piga makofi yenye mahadhi ya regga.

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging