Google PlusRSS FeedEmail

WAKAZI KUTOKA NA ABACUS

MSANII wa miondoko ya Hip Hop nchini Webiro Wassira 'Wakazi' anatarajia kuachia albamu kabla ya albamu 'EP' aliyoipa jina la 'ABACUS' ili kuangalia mapokeo ya muziki huo  kwa mashabiki wake.

Wakazi anatarajia kuitambulisha EP mwishoni mwa mwezi huu ambapo ndani ya albamu hiyo ameshirikisha baadhi ya wasanii wa miondoko ya Hip Hop.

Akizungumza na jarida hii Wakazi aliweka wazi kuwa anachokifanya kuweka ubunifu kuutangaza muziki wake ili uweze kupokelewa na mashabiki wake.

Alisema kuwa njia anayoitumia haijazoeleka katika soko la muziki, ingawa anaamini muziki ili uendelee lazima wakubali kufanya mabadiliko yenye ubunifu.

Alisema kuwa kwa njia ya kutoa albamu kabla ya albamu inamsaidia kutambua mapokeo ya muziki wake kwa mashabiki wake kabla ya kutoa albamu kamili.

Aliongezea kuwa anajiandaa kutoa video ya nyimbo inayojulikana kwa jina la 'Touch' ambapo nyimbo hiyo imeendelea kufanya vizuri na kupokelewa vyema na mashabiki.

Wakazi ni miongoni mwa wasanii waliopata mafanikio kwa kupitia muziki huo ambapo ameweza kutwaa tuzo ya video bora ya mwaka katika Afro Entertainment Awards 2013 nchini Marekani.

This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging