
“Katika soko la filamu kuna tabia ya kubaniana, wasanii wakongwe hawataki kizazi kipya, kila sehemu wanataka wao pamoja na kuwa hawawezi, unamkuta mtu akipewa nafasi ya kukuongelea kwa bosi anakuponda mwanzo mwisho, sasa na sisi tunasema Maveterani wakae pembeni wasubiri mechi za mazoezi,”anasema barafu.
Msanii huyo ambaye pia ni muongozaji wa filamu amedai kuwa mitaani kuna vipaji vingi lakini vinanyimwa nafasia na wasanii wakongwe ambao hawataki kabisa kutoa nafasi kwa wasanii hao ili kuleta ushindani wa kweli katika tasnia ya filamu Swahiliwood, Barafu yupo mbioni kuachia filamu yake inayokwenda kwa jina la Dala dala kutoka kampuni ya Usambazaji ya Leo Media.