
.“Nimetembea na kujifunza mengi wasanii wa Tanzania wengi tuna vipaji vya hali ya juu katika uigizaji lakini inawezekana tatizo letu lipo katika soko letu kwa kazi zetu, nimeongea na mwigizaji wa kimataifa kutoka nchini Ghana Van Vicker amenishauri umuhimu wa wasanii wetu kujua Kiingereza ikiwezekana kurekodi hata filamu itakayotumia lugha hiyo,”anasema Ramsey.
Hivi karibuni msanii Ramsey alimleta msanii kutoka nchini Ghana Van Vicker na kurekodi naye filamu yake akishirikiana naye lengo likiwa kulikata soko la kimataifa au kujenga ushirikiano na msanii huyo kwani awali Mzee Kambi aliwahi kwenda nchini Ghana kushiriki filamu ya Van Vicker akiigiza kama daktari katika filamu hiyo.