Google PlusRSS FeedEmail

AY AOMBA MASHABIKI KUMPIGIA KURA


MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Ambwene Yesaya 'AY' awaomba mashabiki na wadau wa muziki kumpigia kura katika kinyang'anyiro cha tuzo za video za  Channel O Afrika (CHOAMVA).

AY ni miongoni wa wasanii ambaye anajitahidi kuutangaza muziki wa Tanzania katika mipaka ya nje ya nchi, ambapo ni zaidi ya mara moja kutajwa kuwania tuzo mbalimbali nje ya nchi.

Akizungumza na jarida hili msanii huyo amewataka mashabiki na wadau wa muziki nchini kumpigia kura ili aweze kufanikiwa kutwaa tuzo hizo ambapo ametajwa kuingia katika vipengele viwili ikiwemo video ya msanii bora wa kume, na video bora ya Afrika Mashariki.

AY amedai kuwa ili kufanikisha zoezi hilo na kutoa ushawishi kwa mashabiki wake kumpigia kura ameanda shoo itakayofanyika Club Bilicanas jumapili ya wiki hii ili kutoa hamasa kwa mashabiki wake.

"Watanzania wote wenye mapenzi na huu muziki nawaomba wanipigie kura kwa wingi ili niweze kutwaa tuzo hizo ambapo ili kuniwezesha kushinda unaandika ujumbe mfupi kwenye simu yako 1D kwenda namba +2783142100415 hapo unaweza kuniwezesha kuchukua tuzo hiyo" alisema AY.

Amewaomba watanzania kumuunga mkono katika juhudi zake kwa kuutangaza muziki wa Tanzania barani Afrika.





This entry was posted in

Leave a Reply

    Powered By Blogger

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below...

    Get This SpiceUpBlogging